Welcome Note from Commissioner

Mr I. L. KAMUZORA
Commissioner of Insurance

Ndugu mtumiaji wa tovuti hii,

Kwa niaba ya Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA), napenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha katika tovuti ya Mamlaka iliyotengenezwa mahsusi kukupa taarifa mbalimbali kuhusiana na sekta ya Bima. Ni matumaini yetu kuwa, kila atakayefungua tovuti hii atafurahi kupata taarifa kulingana na hitajio lake kuhusiana na huduma za Bima.

 

Tovuti hii hivi karibuni imefanyiwa marekebisho kwa kuongeza kasi ili itumike kwa urahisi katika kupata taarifa. Vile vile, kwa sasa TIRA imeunganishwa na makampuni ya Bima na wadau wengine na mifumo inayofahamika kama  Risk Based Supervision System (TIRA-RBS) na TIRA Motor Insurance Stickers (TIRA MIS)  ambayo inatumika kusimamia na kukagua shughuli za kila siku katika soko la Bima. Pia, wateja wetu wanaweza kuwasilisha malalamiko na maswali kupitia tovuti yetu na hivyo kupata mrejesho stahiki.

 

Nyaraka na taarifa zilizowekwa ni kwa matumizi kwa yeyote atakayetembelea tovuti hii, iwapo tatizo litatokea katika kutumia tovuti yetu tafadhali usisite kuwasiliana na ofisi zetu.

 

Ahsante kutembela tovuti yetu.

I.L Kamuzora

Kamishina wa Bima