Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Semina ya kutoa uelewa kwa Wizara ya Nishati pamoja na Wataalam wa Timu ya Majadiliano ya Kitaifa ya Miradi ya Nishati kuhusiana na Konsotia ya Mafuta na Gesi,
17 Jul, 2023
Semina ya kutoa uelewa kwa Wizara ya Nishati pamoja na Wataalam wa Timu ya Majadiliano ya Kitaifa ya Miradi ya Nishati kuhusiana na Konsotia ya Mafuta na Gesi,

Tarehe 15 Julai 2023 katika ukumbi wa Glan Melia Hoteli jijini Arusha, Semina ya kutoa uelewa kwa Wizara ya Nishati pamoja na Wataalam wa Timu ya Majadiliano ya Kitaifa ya Miradi ya Nishati kuhusiana na Konsotia ya Mafuta na Gesi, Majukumu, Manufaa ya Uendeshaji wa Konsotia pamoja na njisi konsotia inavyoweza kushirki kwenye miradi mbalimbali ya Nishati pamoja na maeneo ya ushirikiano kati ya Wizara ya Nishati, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) na Kampuni za Bima ilifunguliwa na Waziri wa Nishati wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. January Yusuf Makamba, ambapo kampuni 22 za bima zimeungana katika kutatua fursa zilizopo katika miradi ya sekta ya Nishati nchini kama vile majanga katika miradi ya mafuta na gesi.

Akizungumza katika ufunguzi wa semina hiyo, Waziri wa Nishati Mhe. January Yusuf Makamba ameyataka makampuni ya bima nchini kuja na ujuzi na maarifa ili kuzikimbilia fursa zilizopo katika sekta ya nishati hatimaye kukuza mchango wa sekta ya bima katika uchumi wa Taifa.

Kwa upande wake Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo Saqware amesema, konsotia ya mafuta na gesi ilizinduliwa rasmi tarehe 16 Novemba 2022 na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Chande. Aidha, amesema kuwa lengo la konsotia hiyo ni kuhakikisha uandikishaji wa majanga kwenye miradi ya mafuta na gesi nchini unaanzia angalau asilimia 45% ili kuleta tija kwa nchi na uchumi kwa ujumla.

Semina hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo Waziri wa Nishati, Mhe. January Yusuf Makamba, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Athumani Mbuttuka, Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo Saqware, Naibu Kamishna wa Bima Bi. Khadija I. Said, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Dunstan Luka Kitandula, Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Iddi Kassim Idd, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Mhandisi. Charles Sangweni, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Daniel Sillo, Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Dkt. Charles Kimei na Mhe. Zaituni Swai, Kamishna Msaidizi sehemu ya Maendeleo ya Petroli Wizara ya Nishati Marwa Petro, Mwenyekiti wa Umoja wa Kampuni za Bima (ATI) Bw. Khamis Suleiman pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya bima na nishati.

“HONGERENI SANA WADAU WA SEKTA YA BIMA KWA MAFANIKIO MAKUBWA 2023”