Darasa ndani ya Kijiji cha Bima: Wanafunzi wapewa elimu ya bima ndani ya Maonesho ya Saba Saba
09 Jul, 2025

Wanafunzi kutoka Kilimani Schools leo Julai 9, 2025 wamepatiwa elimu ya bima ndani ya Maonesho ya Saba Saba ikiwa ni mwendelezo wa utoaji elimu kutoka TIRA ambapo pia kampuni mbalimbali za bima zimeshiriki katika darasa hilo la bima.
Wanafunzi pia walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali yaliyojibiwa kwa ufasaha kutoka kwa wataalamu wengi wa bima walioshiriki kutoa elimu hiyo.
Pia walimu walioambatana na wanafunzi hao wameishukuru Mamlaka kwa nafasi waliyoipatia shule hiyo na kuahidi kuendeleza ushirikiano ili wanafunzi wengi wa ngazi za chini waweze kufahamu umuhimu wa bima na kuwa mabalozi kwa wengine.
TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA