Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mh. Dkt. Doto Biteko leo Septemba 19, 2023 amekutana na Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware
19 Sep, 2023
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mh. Dkt. Doto Biteko leo Septemba 19, 2023 amekutana na Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mh. Dkt. Doto Biteko leo Septemba 19, 2023 amekutana na Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware pamoja na Naibu Kamishna Bi. Khadija Said ambao waliambatana na Mabalozi wa Bima, Viongozi wa TIRA Pamoja na Kamati ya Ufundi ya Konsotia ya Mafuta na Gesi wamefanya mazungumzo yenye lengo la kutoa fursa kwa kampuni za Bima zilizosajiliwa nchini kushiriki katika uchumi wa mafuta na gesi.

Kamishna wa Bima amemueleza Dkt. Biteko kuwa Konsotia ya Bima iliyozinduliwa Novemba 2022 inaundwa na umoja wa Makampuni 22 ya Bima yenye mtaji wa jumla ya Dola za Kimarekani Mil. 6. Aidha kamishna ameeleza kuwa malengo ya Mamlaka na Konsotia kwa ujumla ni kuhakikisha miradi yote ya gesi na mafuta inabakiza sio chini ya 45% ya ada zinazotokana na mafuta.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Said amesema, Sekta ya bima nchini imejidhatiti katika kuweka uwekezaji mkubwa ili kuvutia miradi mikubwa nchini na nje ya nchi kukata bima kwenye kampuni za hapa nyumbani ili fedha hizo zibaki nchini na hatimae kukuza uchumi na kwamba serikali iziamini kampuni hizo na kufanya nazo biashara.

Mhe. Naibu Waziri Mkuu ameuhakikishia ujumbe huo wa Sekta ya Bima kuwa Serikali inaamini katika kuwajengea uwezo wazawa ambao wanaonyesha uwezo katika maeneo mbalimbali ikiwemo hii sekta ya bima na kuwataka kuendelea kuwa wabunifu katika biashara zao na kwamba Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano stahiki.

Nao Mabalozi wa Bima Mh. Japhet Hasunga na Mh. Wanu Ameir kwa upande wao wamemshukuru Mh. Dkt. Biteko kwa kufungua Milango kwa Makampuni ya Kitanzania ya Bima kutumia fursa zilizopo nchini na Jirani kuimarisha biashara zao.

Kampuni zinazounda Konsotia ya Mafuta na Gesi ni 22 ambapo TanRE ni Msimamizi wa Konsotia huku Phonex ikiwa ni Kampuni kiongozi.