Utoaji elimu ya bima; TIRA yashiriki Maonesho ya Kitaifa ya Kazi za Utamaduni na Sanaa

Aprili 25, 2025
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania imeungana na taasisi mbalimbali kushiriki Maonesho ya Kitaifa ya Kazi za Utamaduni na Sanaa kama jukwaa la kutoa elimu ya bima kwa wananchi mbalimbali wanaotembelea mabanda ya maonesho, lengo kubwa ikiwa ni kufikisha elimu ya bima kwa wananchi. Maonesho hayo yalianza rasmi hapo jana tarehe 24 Aprili 2025 na yanatarajiwa kumalizika Aprili 30, 2025 katika viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam.
Akifungua Maonesho hayo yaliyoandaliwa na Mfuko wa Utamaduni Tanzania, Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Metheusula Ntonda amezipongeza Taasisi zilizoshiriki katika kuendeleza kazi za Utamaduni na Sanaa lakini pia Mhe. Ntonda alielezwa shughuli mbalimbali za Mamlaka alipotembelea banda la Mamlaka hiyo, zikiwemo kusajili na kutoa leseni kwa watoa huduma za bima, kuandaa na kutoa kanuni na miongozo mbalimbali kusimamia soko la bima, kutoa elimu ya bima kwa umma, kulinda haki za mteja wa bima lakini pia kuishauri Serikali juu ya masuala ya bima, na kuipongeza Mamlaka kwa kazi nzuri ya uelimishaji.
Wananchi wote mnakaribishwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja kupata elimu ya bima na ikiwa una changamoto yoyote ya kibima unakaribishwa, tunakusikiliza na tunatatua.
TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA