Kaimu Afisa wa Usalama Barabarani wa wilaya ya Kahama Bw. G. Kaigwa akifurahi jambo na askari wake wakati mafunzo ya matumizi ya TIRA MIS yaliyokuwa yakitolewa na Bi Adelaida Muganyizi (Mkurugenzi wa Uendelezaji Masoko na Utafiti - TIRA) na Bw. Arthur Mbena (Mwanasheria - TIRA). Mafunzo hayo yalifanyika tarehe 24 Mei 2017 katika kituo kikuu cha Polisi cha Kahama na kufuatiwa na operesheni maalumu iliyofanyika katika barabara kuu za mjini huo ili kubaini vyombo vya moto vyenye bima bandia.