Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh Dk. Leonard Masale akionyeshwa jinsi ya kuhakiki bima za vyombo vya moto mara baada ya kuzindua mafunzo na matumizi ya TIRA MIS jijini Mwanza tarehe 26 Mei 2017 na kuwataka wadau wote wa bima kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima katika kutokomeza udanganyifu unaofanya na wafanyabiashara wasio waaminifu kwa kuwauzia wamiliki wa vyombo vya moto bima bandia. Pia Dk Masale aliwataka wamiliki wa vyombo vya moto kuhakiki bima zao kabla hawajaondoka kwenye kampuni, dalali au wakala aliyemkatia bima ili kuondoa utata pale bima inapokutwa ni bandia na hivyo kumsababishia hasara mmiliki. Kwa kutumia mfumo wa TIRA MIS, mmiliki wa chombo cha moto anaweza kuhakiki bima yake kwa kutumia simu ya mkononi au  kwa kufungua tovuti ya TIRA MIS na kisha kuhakiki taarifa zake kwa wepeni na haraka.