Mamlaka ya Kusimamia Shughuli za Bima Nchini (TIRA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Bima Tanzania imetoa mafunzo ya kutumia mfumo wa kielektroniki wa kulipia bima za mizigo inayoingizwa nchini kupitia njia ya bandari, barabara, reli na anga. Mfumo huu umeanzishwa ili kukidhi matakwa ya marekebisho ya sheria yaliyofanyika mwaka 2017 kuhusu mizigo inayoingizwa nchini.

Katika mafunzo hayo, makampuni ya bima, Madalali na Wasahuri wa Bima pamoja na Mawakala kutoka mkoa wa Mwanza, Shinyanga, Geita, Kigoma, Kagera, Simiyu na Mara walihudhuria.