Mamlaka ya bima nchini imeendelea kutoa elimu ya bima kwa makundi mbalimbali nchini ili kuhakikisha huduma hii inawafikia watanzania wengi. Mamlaka imewataka wanachama wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) kuhakikisha wanatumia huduma na bidhaa mbalimbali zitolewazo na makampuni ya bima nchini.

Pia, katika mkutano huo Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Nchini iwaeonyesha wafanyabiashara hao jinsi mfumo wa kulipa bima za mizigo inayoingizwa nchini unavyofanya kazi. Sambamba na hilo, Mamlaka imeeleza ni namna gani mfumo huu wa Tanzania Imports Insurance Portal kupiti tuvuti ya (www.tiip.co.tz) unaleta faida kwa taifa na soko la bima (makampuni, wafanyabiasha, na mwananchi mmoja mmoja anayeagiza mizigo kuingiza nchini).