Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Nchini (TIRA) leo imewasilisha hundi ya kiasi cha Bilioni Moja Milioni Mia Tatu Hamsini na Sita, Laki Tatu Sitini na Sita elfu Mia Mbili Hamsini (Tsh. 1,356,366,250/=) kwa Mh. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika hafla ya makampuni na taasisi za serikali zinayopaswa kutoa gawio na kuchangia sehemu ya mapato yake katika Mfuko Mkuu wa Serikali. TIRA ni miongoni mwa mashirika, taasisi na wakala waserikali arobaini na saba (47) zilizotoa hundi kwa mheshimiwa rais.