WIKI YA BIMA ZANZIBAR YA YAWAFIKIA WAZEE.

Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini (TIRA) kwa kuishirikiana na makampuni yanayotoa huduma za bima nchini wanaadhimisha wiki ya bima kwa upande wa Zanzibar.

Katika kuhakikisha kuwa huduma za bima zinawanufaisha watanzania wengi hasa wenye uhuhitaji maalumu Mamlaka ya Bima imepanga kutemebelea wagojwa kwenye Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Kituo cha Kulelea wa Wazee cha Sebuleni na Kituo cha Kulelea Watoto yatima Mazizini.

Akizungumza na wazee wanaopata huduma katika kituo hicho, Mkurugenzi wa Soko na ufuatiliaji Bw. Elia Kajiba alisema tumefika katika kituo hiki kwa kuheshimu na kuthamini juhudu za wazee hawa wakatika wa ujana wao.

Wazee ni shemu ya mafanikio ya nchi yetu kwani mpaka nchini ilipofikia kwa sasa ni mjumuisho wa jitihada za wazee hawa, na kwa namna nyingine mafanikio ya makampuni ya bima ni matunda ya juhudi za hawa wazee.

“Hii inadhihirisha jinsi sekta ya Bima anavyokuwa moja ya nguzo muhimu katika ustawi wa jamii. Hivyo, kwa kurudisha kile tunachokipata kwa jamii ni kuhakikisha jamii yetu inakingwa na kurejeshwa katika hali ya nzuri ya maisha” alisema Bw. Kajiba.

Akitoa salamu za shukurani, Naibu Katibu Mkuu Wizara za Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Bi. Mwajuma Majid amesema kuwa sekta ya bima inapaswa kuendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri za bima.

“Wazee hawa leo wanapata huduma hapa chini ya uangalizi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar nikiri kufurahia msaada huu tulioupata kutoka kwa Mamlaka ya Bima kwa kushirikiana na makampuni wanayoyasimamia” alisema Bi. Mwajuma.

Miongoni mwa vifaa vilivyotolewa kwa wazee hao ni pamoja na mashuka, vyombo vya chakula, chupa za chai na pasi kulingana na uhitaji wao.

Shughulizi hizi za wiki ya Bima kwa upande wa Zanzibar itafanyika kwa siku tatu na kufikia kilele chake tarehe Jumamosi ya Tarehe 23, Juni 2018 kwa maandamano ya amani yatakayoanzia viwanja vya Komba Wapya na kuishia viwanja vya Mapinduzi kwaajili ya kutoa kutoa elimu ya bima na kutatua changamoto za bima.