Naibu Waziri wa Ardhi Mh. Anjelina S.L. Mabula (Mb) akipata maelezo matumizi ya mfumo wa kuhakiki bima za vyombo vya moto (TIRA MIS) kutoka kwa Mkurugenzi wa Uendelezaji Masoko na Utafiti Bibi. Adelaida Muganyizi katika Maonyesho ya NaneNane yanayofanyika Kitaifa Ngongo, Mkoani Lindi na kutoa wito kwa Mamlaka kuendelea kutoa elimu hii kwa wananchi wengi zaidi ili wajiunge na biashara ya bima au watumie huduma na bidhaa za bima kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.