Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima imezindua Tuzo za umahiri katika sekta ya Bima (excellence in Insurance Sector) zitakazofanyika kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu kuanzia leo na kufikia kilele chake Septemba 27, 2019 jijini Mwanza. Mchakato wa kuanza kupokea maobi ya washiriki kutoka katika sekta ya umma yamefunguliwa rasmi leo.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo A. Saqware alisema katika tuzo hizi zawadi zitajumuisha, Vikombe, Vyeti vya Utambuzi na Barua za Utambuzi kutoka kwa Mamlaka na wadhamini mbalimbali kulingana na kila kipengele. Pia, tuzo zitatolewa kwa Mshindi wa Kwanza, Mshindi wa Pili, na Mshindi wa tatu huku baadhi ya Tuzo zitakuwa na Mshindi mmoja.

Zoezi la kupokea naombi litahhusisha vipengele vyote vitano ambavyo ni Tuzo ya Umahiri katika Elimu kwa Umma (Insurance Awareness Campaign of the Year); Tuzo ya Umahiri katika Elimu kwa Umma (Insurance Awareness Campaign of the Year); Tuzo ya Umahiri katika Kutoa Huduma kwa Jamii (Corporate Social Responsibility (CSR); Tuzo ya Umahiri kwa Kijana anayeibukia (Umri miaka 18-30) (Insurance Young Achievers Awards) ambayo itatolewa kwa kijana aliyefanya vizuri katika Ujasiriamali na kijana aliyefanya vizuri katika Utafiti unaohusisha urahisi wa upatikanaji wa huduma za bima.

Pia, tuzo zingine ni tuzo ya Umahiri katika bidhaa bora na yenye ubunifu (Most innovative Insurance Product); na Tuzo ya Kampuni Bora ya Mwaka (Insurance Registrant of the year Award).

Nyaraka na fomu za maombi ya kushiriki katika mchakato huu zinapatikana katika www.insuranceawards.or.tz