Ubunifu wa bidhaa mpya za bima ni muhimu kakitka kuchochea ukuaji wa soko la bima nchini sambamba na kusogeaza huduma kwa Wananchi walio wengi hususan vijijini. 

Hayo yamesemwa na na Kamishana wa Bima Nchini Dkt. Baghayo Abdalah Saqware wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa bidhaa ya mpya ya bima iliyobuniwa na kampuni ya Bima ya Jubilee inayofahamika kama kifurushi cha bima ya maduka “dukani package insurance” kwa lengo la kukinga majanga kwa wenye maduka pamoja na mteja anapokuwa akihudumiwa.

Kamishna Dkt. Baghayo alisema bima hizo zitawafikia haraka watumiaji kwa kuwa zinazingatia teknolojia ambayo itarahisisha upatikanaji wa hiyo huduma kwa watumiaji. Amongeza kuwa bidhaa zilizobuniwa zinawalenga watu wa kawaida na zinaendana na mahitaji ya serikali ya kupanua wigo wa huduma za bima nchini.

Mkuu huyo alifafanua kuwa huduma hii ikweza kuyafikai maduka mengi nchini kuanzia miji mikubwa mpaka wilayani tutakuwa tumeongeza huduma ya upatikanaji wa bima hapa nchini ambayo I kinga muhimu kwa biashara na kwa mtu mmoja mmoja.

“Mamlaka itaedelea kuwashauri na kupitia mapendekezo ya bidhaa zenu kwa haraka kwa ajili ya kutoa vibali,” alisema Dkt. Saqware.

Alisisitiza kuwa bidhaa zinazotolewa ziwalinde wateja wanaopelekewa wanaotumia huduma hiyo akirejea jinsi ambayo itakuwa inapatikana kwa teknolojia ya mtandao, haraka na kuondoa malalamiko.

Ameahidi kuwa Mamlaka itaendelea kuweka mazingira wezeshi na haraka kwa kampuni za bima katika kusajili bidhaa mpya za bima hususan zinaziwalenga Wananchi wa kipato cha chini.