Wafanyakazi wa TIRA washiriki matembezi ya kuhamasisha na ku elimisha umma wa Tanzania juu ya huduma na bidhaa  zinazotolewa na madalali wa bima nchini(Insurance Awareness Walk). Matembezi haya yaliandaliwa na kudhaminiwa na Kampuni ya bima mtawanyo yaani Tan-RE pamoja na umoja wa madalali wa bima Tanzania (TIBA) ikishirikiana na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Wadau wa bima zaidi ya mia mbili na hamsini walishirki matembezi  haya yaliyofanyika tarehe 29 Julai 2017 yaliyoanzia Chuo cha Usimamizi wa Fedha hadi Maktaba Kuu ya Taifa ambapo ofisi za TIBA zilipo.