Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) wameungana na wafanyazi kote nchini kusherehekea Sikukuu ya Wafanyakazi ya Mei Mosi iliyofanyika kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Mgeni Rasmi katika sherehe hizo, alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye katika hotuba yake kwa wafanyakazi nchini aliwataka kufanya kazi kwa bidii katika maeneo yao huku akiahidi kuwa wawe wavumilivu wakati Serikali inashughulikia uboreshaji wa maslahai yao.

Shughuli za Mei Mosi mwaka huu 2022 zilibebwa na kauli mbiu isemayo“ Mishahara na Maslahi Bora kwa Wafanyakazi Ndio Kilio Chetu: Kazi Iendelee”.

Wafanyakazi wa TIRA walishiriki katika sherehe za kitaifa zilizofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma pamoja na Uwanja wa Uhuru katika maadhimisho yaliyofanyika kimkoa jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa Bima nchini alituma salaam za kuwatakia Wafanyakazi wa TIRA na wananchi kwa ujumla maadhimisho mema ya sikukuu ya mei mosi.