Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) cha Jijini Dar es Salaam wamepata mafunzo ya miongozo ya bima iliyotolewa hivi karibuni kwa ajili ya kuendeshea soko la bima nchini.

 

Mafunzo hayo yametolewa kwa wananfunzi wa Kitivo cha Bima na Hifadhi ya Jamii (Faculty of Insurance and Social Protection) katika mhadhara ulioandaliwa na uongozi wa Kitivo hicho kuihusu Mkakati wa Sekta ya Bima katika kufikia huduma za fedha jumuishi.

 

Miongozo iliyotolewa ufafanuzi na jinsi ya kuitumia kupata fursa ya kushiriki katika kufanya biashara ya bima ni pamoja na Miongozo ya Maafisa Wauza Bima, Utoaji Huduma za Bima Kidijitali na  Uendeshaji wa Takaful.

Akitoa mhadhara kwa wananfunzi hao Kamishna wa Bima nchini Dkt. Baghayo Saqware amesema miongozo hiyo ni fursa kwa wananfunzi kuweza kuingia katika soko la bima na kutoa huduma kwa Wananchi hata kabla ya kumaliza masomo yao.

Kamishna wa Bima amesema miongozo hii ieka kwa wakati muafaka kwai itasaidia wataalamu wa bima kwa kushirikiana na taaluma zingine kuja na bidhaa ambazo zitawafikia wananchi kwa urahisi.

Pia, Wanafunzi wamefahamishwa kuwa Ofisi ya Kamishna wa Bima iko tayari kutoa ushauri kwa wananfunzi hao pindi yeyote anapotaka kufungua biashara ya bima.

Naye Mkuu wa Kitivo cha Bima na Hifadhi ya Jamii wa IFM Dkt. Johh Kingu ameishukuru Mamlaka kwa kukubali kushiriki katika  mhadhara huo ambao amesema una tija kubwa kwa wananfunzi waliohudhuria.

Huu ni mwanzo wa mihadhara kama hii na itaendelea kutolewa katika vyuo mbalimbali ili kuwatengeneza vijana kuwa mahiri na weledi wakati wa kutoa huduma za bima kwa Wananchi.