Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
DKT. BAGHAYO SAQWARE ATOA ELIMU KUHUSU BIMA KWA MAAFISA UNUNUZI
13 Dec, 2023
DKT. BAGHAYO SAQWARE ATOA ELIMU KUHUSU BIMA KWA MAAFISA UNUNUZI

Leo tarehe 13Desemba 2023, Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware ametoa  elimu kuhusu bima kwa Maafisa ununuzi wanaoshiriki  Mkutano wa 14 wa Wataalam   wa Ununuzi na Ugavi unaofanyika Jijini Arusha. Kamishna kwenye Mkutano huo  ameambatana na Watumishi wengine wa Mamlaka ( TIRA). Mapema jana Desemba 12, 2023 Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba alitembelea banda la TIRA na kupewa maelezo juu ya shughuli za TIRA na Sekta ya bima kwa Ujumla. TIRA-kwa Soko Salama la Bima.