Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Tunachofanya

 Majukumu ya Mamlaka. 

  • Kusajili kampuni za bima nchini;
  • Kusimamia na kukagua mwenendo wa kampuni za bima nchini;
  • Kushughulikia malalamiko ya wananchi dhidi ya huduma za bima;
  • Kutoa elimu ya bima kwa umma;  na
  • Kusimamia biashara ya bima na masula yanayohusika na bima kwa mujibu wa sheria.

Kuhusu TIRA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), chini ya Sheria ya Bima Na.10 ya mwaka 2009, ni taasisi ya serikali ilioanzishwa ili kutekeleza majukumu ya kusimamia soko na kuendeleza biashara ya bima nchini na masuala yanayohusiana na bima kwa mujibu wa sheria ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tunaowahudumia

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania inahudumia kampuni za bima zilizosajiliwa, wadau wote na umma kwa ujumla wa bima kwa mujibu wa sheria.