Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
MATEMBEZI YA BIMA 2022
05 Nov, 2022 07:00 - 10:00 am
IIT OFFICES TO MNAZI MMOJA GROUNDS
eliezer.rweikiza@tira.go.tz

Mamlaka ya Usimamizi  wa Bima Tanzania (TIRA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) wameandaa matembezi ya bima yatakayofanyika Jumamosi tarehe 5 Novemba 2022 jijini Dar es Salaam yakilenga kujenga uelewa wa bima na  kukuza huduma za bima nchini. Matembezi hayo yatahusisha wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), watoa huduma za bima, wafadhili pamoja na maafisa wa Serikali. Matembezi haya yatafunguliwa na Kamishna wa Bima Dkt.Baghayo Abdallah Saqware na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ng'wilabuzu Ndatwa Ludigija. Njia itakuwa: Ofisi za IIT - Uhuru Heights - Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) - Askari Monument - Clock Tower - kuishia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja. Baada ya hapo, kongamano la wazi la bima na maonyesho vitaendelea katika viwanja hivyo ambapo inategemewa wananchi wa mkoa wa Dar es salaam watapata fursa ya kutembelea viwanja hivyo na kupata uelewa wa masuala ya bima na taratibu zake. 


 
MATEMBEZI YA BIMA 2022