Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
UZINDUZI WA TAARIFA YA UTENDAJI WA SOKO LA BIMA NCHINI KWA MWAKA 2023
22 Nov, 2024 2.00 AM - 06.00
SUPERDOME MASAKI
anna.massao@tira.go.tz, tabiamchakama@tira.go.tz

Kamishna wa Bima afanya mkutano na vyombo vya habari; aeleza yaliyoshehena Uzinduzi wa Taarifa ya Soko la Bima nchini 2023

Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware Novemba 13, 2024 amefanya mkutano na vyombo vya habari mbalimbali kuzungumzia Uzinduzi wa Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima nchini kwa mwaka 2023 utakaofanyika katika ukumbi wa The SuperDome Masaki jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Novemba 2024.

Kamishna alianza kwa kuelezea umuhimu wa bima kwa wananchi pale wanapokumbwa na majanga mbalimbali, “Bima ni bidhaa au huduma ambayo inatoa kinga kwa mali za aina mbalimbali afya na uwekezaji, endapo majanga ya kiuchumi au kijamii yatatokea bima hutoa fidia na kinga”alisema.

Dr. Saqware pia alieleza umuhimu wa Taarifa hiyo ya Utendaji wa Soko kwa mwaka 2023 kwamba imeeleza kuhusu ukwasi wa soko, uhimilivu wa soko, uwajibikaji wa wananchi kulipa madai, utendaji wa soko kwa ujumla lakini pia taarifa inaeleza taarifa za waliosajiliwa  kutoa huduma hizo za bima hapa nchini.

Lakini pia Kamishna alieleza uandikishaji wa ada za bima umekua kwa mwaka 2022 ilikua trilioni 1.1 na kwa mwaka 2023 imepanda hadi trilioni 1.2 na hivyo kuonyesha ukuaji wa soko la bima.

Kamishna alimalizia kwa kuwakaribisha wadau wote wa sekta ya bima katika mkutano huo.

UZINDUZI WA TAARIFA YA UTENDAJI WA SOKO LA BIMA NCHINI KWA MWAKA 2023