Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Mkutano wa 18 wa  Wasimamizi na Wakuu wa Mamlaka za Bima kwa  Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
05 Apr, 2023
Mkutano wa 18 wa  Wasimamizi na Wakuu wa Mamlaka za Bima kwa  Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Mkutano wa 18 wa  Wasimamizi na Wakuu wa Mamlaka za Bima kwa  Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (East Africa Insurance Supervisors Association (EAISA) ) uliofanyika kuanzia tarehe 30 hadi 31 Machi 2023 ambapo Uganda ilikuwa Nchi mwenyeji.

Pichani ni wakuu wa mamlaka za bima waliohudhuria mkutano huo.Kutoka kushoto ni: Kamishana wa Bima-Tanzania  akifuatiwa na Makamishna wa bima wa Kenya,Uganda, Mwenyekiti wa Bodi ya IRA Kenya,akifuatiwa na mwakilishi wa Gavana Benki Kuu ya Rwanda na  General Secretary ARCA ya Burundi.

Mkutano huo hufanyika kila mwaka na Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kujadiliana masuala mbalimbali hasa namna ya kushirikiana kuendeleza soko la bima kwa nchi wanachama.

Kwa upande wake, Dkt. Baghayo Saqware,aliwaeleza washiriki kwamba,nimuhimu kujadiliana na kushirikiana kwa sababu soko la bima kwa nchi za ukanda wa Afrika mashariki lina maeneo mengi yanayofanana hivyo hata changamoto na utatuaji wake vinaendana na zinahitaji juhudi za pamoja katika utatuzi wake.