Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Afya na Kazi, Kazi na Michezo TIRA yashiriki mashindano SHIMMUTA 2024 Tanga
14 Nov, 2024
Afya na Kazi, Kazi na Michezo TIRA yashiriki mashindano SHIMMUTA 2024 Tanga

Michuano ya michezo  ya SHIMMUTA inaendelea mkoani Tanga ambapo wanamichezo mbalimbali kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA)  wanashiriki. Michezo hiyo imeandaliwa na Shirikisho la Michezo ya Umma Taasisi na Makampuni Binafsi (SHIMMUTA).

Baadhi ya michezo ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa pete, bao, ‘pooltable’, karata, riadha’na darts. Akizunguza kuhusu ushiriki wa Mamlaka katika michuano hiyo hiyo Afisa Tawala kutoka TIRA, Bw. Henry Bayona kwa niaba ya Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu , Bi. Hawa Mniga, amesema ‘’Afya na kazi, kazi na michezo, tunashiriki michezo hii kwasababu ni muhimu kwa afya zetu za mwili na akili lakini pia hutuleta pamoja kama wanamichezo na watumishi lakini pia tunaahidi ushindi”.

Jumla ya wanamichezo 4,700 wanashiriki kuanzia Novemba 10 – 24 2024 yatakapomalizika. Mashindano hayo yanatarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 18, Novemba 2024 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko.     

Pia Mkuu wa Wilaya ya Tanga Bw. Japhari Kubecha amesema Serikali ya Wilaya itaendelea kutoa ushirikiano wa bega kwa bega na viongozi wa mashindano hayo ya SHIMMUTA pamoja na taasisi zinazoshiriki na kuwapa ushirikiano wa michezo na kijamii. Amesema hayo alipotembelea uwanja wa bandari kushuhudia michezo mbalimbali iliyokuwa inaendelea.

#TIRA KWA SOKO LA SALAMA LA BIMA NCHINI