Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
BIMA NDIO AFYA, NDIO UCHUMI NA NDIO MAENDELEO - DKT. SAQWARE
05 Aug, 2024
BIMA NDIO AFYA, NDIO UCHUMI NA NDIO MAENDELEO - DKT. SAQWARE

Leo tarehe 5 Agosti 2024 Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo Saqware akiambatana ujumbe wake katika ziara ya kutoa elimu ya bima na kuhamasisha matumizi ya bidhaa na huduma za bima katika nyanda za juu kusini wameshiriki katika Semina ya Vijana na Makundi mbalimbali ya jinsi ya kupambana Kiuchumi katika Wilaya ya Momba, Mkoa wa Songwe.

Tukio hili pia limehudhuriwa na Mbunge wa Momba Mhe. Condester Sichalwe ambaye ameunga mkono zoezi hilo akisisitiza umuhimu wa wanamomba kufikiwa na elimu ya bima ili waweze kuwelewa umuhimu wa kuwa na bima katika maisha yao ili waweze kujikwamua kiuchumi wakiendesha shughuli zao kwa uhakika na wakijiamini.

Aidha, mambo ambayo Dkt. Saqware amewasihi wakazi wa Momba kuipokea elimu hiyo ya bima na kuitumia ili wanufaike na huduma za bima. Maeneo muhimu ambayo huduma za bima ni za muhimu kwa shughuli za wanamomba ni bima za Kilimo, bima za afya na bima za vyombo vya moto.

Dkt. Saqware amewahimiza wanamomba kuchukua hatua ya kujikinga na bima kwani bima ndio afya, ndio uchumi na ndio maendeleo. Unapokijinga na madhara yanayoweza kuibuka bila kutarajia 

Aidha, Mhe. Sichalwe kupitia Semina hii ametoa rai kwa wakazi wa Momba wawe mstari wa mbele kuhakikisha wananufaika na bima. Hii pia ni fursa kwao kuwnzisha vikundi mbalimbali vya maendeleo na hata k