Matembezi ya bima
Leo tarehe 08.07.2023 wadau wa bima na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam wamefanya matembezi ya bima yaani “Bimawalk”. Matembezi hayo yameandaliwa na Chuo cha Bima Nchini (IIT) kwa kushirkiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya bima.
Katika matembezi hayo yenye lengo la kuhamasisha umuhimu wa bima kama kichocheo katika kukuza na kuendeleza uchumi wa Nchi yalianzia Mlimani city mnamo saa mbili asubuhi ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila ameshiriki kama mgeni rasmi. Adha, Kamishna wa Bima Nchini Dkt. Baghayo Saqware ameshiriki pamoja na viongozi mbalimbali wa Mamlaka, kampuni za bima, wadau wa sekta ya bima na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.
“TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA”