Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
CHAMA CHA WAFANYAKAZI TUGHE TAWI LA TIRA; CHAPATA VIONGOZII WAKE, KUENDELEZA MSHIKAMANO NA UMOJA KAZINI
21 Oct, 2024
CHAMA CHA WAFANYAKAZI TUGHE TAWI LA TIRA; CHAPATA VIONGOZII WAKE, KUENDELEZA MSHIKAMANO NA UMOJA KAZINI

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kupitia Chama cha Wafanyakazi TUGHE wanaofanya kazi Mamlaka ya Usimamizi wa Bima TIRA leo tarehe 18 Oktoba 2024 wamefanya Uchaguzi wa Kumteua Mwenyekiti, Katibu na Mjumbe wa Halmashauri wa chama cha wafanyakazi TUGHE wa Mamlaka hiyo (TIRA).

Katika kinyang'anyilo hicho aliyeibuka kidedea kuwa Mwenyekiti ni Ndg. Sausi Mwita Sausi ambaye ni Afisa Bima Kitengo cha Ukaguzi (Inspection) katika  Mamlaka hiyo.

Naye Bi. Victoria Mwavilenga ambaye pia ni Afisa Bima Kitengo cha Leseni ndiye aliyeibuka kidedea kwenye nafasi ya Katibu wa TUGHE na Bwana Halfan Isango, Afisa Bima Kanda ya Ziwa Mwanza aliibuka na Cheo cha Mjumbe  Halmashauri  ya TUGHE TIRA.

Akitoa salamu za Naibu Kamishna wa Bima, Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka Bwn. Ponziano Lukosi amesema, kwa mujibu wa sheria ya Ajira na Mahusiano kazini, kazi ya TUGHE ni kumshauri na kumsaidia Mwajiri katika kujenga mahusiano mazuri kati ya Taasisi na wafanyakazi kwa maslahi mapana ya Nchi.

Kiongozi huyo pia aliwaasa   watumishi wafanye wajibu wao sehemu ya kazi lakini pia amekumbushia  watumishi wa TIRA washiriki kwenye zoezi linaloendelea nchini la  kujiandikisha katika daftari la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili washiriki uchaguzi huo ifikapo tarehe 27 Novemba 2024, kwani sisi watumishi wa Serikali ni mfano wa kuigwa na jamii inayotuzunguka huko mitaani kwetu.

Tukio hilo la uchaguzi wa Viongozi wa TUGHE umefanyika kwenye Hotel ya CROWNE PLAZA Jijini Dar es salaam.

TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA