PALIPO NA HUDUMA YA BENKI, BIMA INAPATIKANA: PBZ SASA RASMI WAKALA WA BIMA
Naibu Kamishna wa Bima, Bi. Khadija Said amezindua rasmi huduma ya benki wakala wa bima ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ Bancaasurance) leo tarehe 23 Julai 2024 Zanzibar.
Hafla hiyo fupi imewaleta pamoja wadau wa sekta ya bima wakiwemo kampuni za bima ambazo zitashirikiana na PBZ kutoa huduma za bima kupitia benki.
Benki ya PBZ imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo kwani sasa huduma za bima zitakuwa zinapatikana kwenye matawi yote ya PBZ yaliyopo mijini na vijijini kauli kuu ikiwa “Palipo na huduma ya benki, Bima inapatikana”.
Huduma ya Benki wakala wa Bima nchini imeendelea kukua kwa kasi hadi kufikia asilimia 15 kwa mwaka huu pekee. Hii inaonyesha jinsi gani huduma hii imepokelewa vema na wananchi.
“Hali hii inaleta matumaini makubwa kwamba tuko kwenye njia sahihi ya kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata huduma bora za bima kupitia benki wakala”, amesema Naibu Kamishna wa Bima, Bi. Khadija Said.
Aidha, Bi. Khadija amewataka Benki wakala wa bima wote kufuata miongozi iliyowekwa katika kutoa huduma za benkibima ili soko la bima likibakia kuwa endelevu.
Naibu Kamishna pia amezipongeza kampuni za bima ambazo tayari zimeshajiunga na PBZ lakini pia amewasisitiza wale ambao bado hawajajiunga na PBZ wafanye hivyo ili kuongeza ushindani zaidi katika kutoa huduma Bora za Bima kwa watanzania.
#TIRAKwaSokoSalamalaBima #BimaTanzania #ElimuYaBima #MtejaKwanza #BimaNiMuhimu #BimaNiSalama