Ugawaji wa Hundi kwa Wakulima wa Tumbaku
Leo Tarehe 07 Agosti 2023, Mkurugenzi waTafiti na Masoko wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania, Ndugu Samweli Mwiru wa kwanza kulia ameshiriki Ugawaji wa Hundi kwa Wakulima wa Tumbaku yenye thamani ya dola za Kimarekani elfu 33,537,88/= ambazo zinakadiriwa kuwa Shilingi milioni 80,000,000/= pesa za Kitanzania. Hundi hiyo ilitolewa na Benki Wakala ya NBC kupitia Kampuni ya Bima ya Jubilee Allianz chini ya Mkurugenzi wake Ndugu. Bipankar Acharya wa tatu kulia. Hafla hiyo fupi iliyofanyika kwenye Ukumbi wa JKT ndani ya viwanja vya Nanenane Jijini Mbeya, ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa Kilimo na Bima wakiwemo wajumbe wa vyama vya Ushirika. Mkurugenzi huyo wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima aliwaasa Wakulima kuendelea kutumia huduma za Bima za Kilimo kwa kuwa hufidia hasara pindi zinapojitokeza kama tunavyoshuhudia leo hii na Kilimo kina changamoto nyingi sana.
TIRA- kwa Soko Salama la Bima.