Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
DKT. SAQWARE AFUNGUA MILANGO ZAIDI KWA MAWAKALA WA FORODHA TANZANIA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO NA TIRA
21 Oct, 2024
DKT. SAQWARE AFUNGUA MILANGO ZAIDI KWA MAWAKALA WA FORODHA TANZANIA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO NA TIRA

Octoba 18, 2024 katika ukumbi wa  Karimjee jijini Dar es Salaam, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kupitia Kanda ya Mashariki imekutana na mawakala wa forodha Tanzania ambao ni wanachama wa TAFFA na TACAS katika semina maalumu iliyolenga kutoa elimu kuhusu bima. 

Mgeni Rasmi katika semina hiyo alikuwa Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware ambapo alifungua rasmi mafunzo hayo na kuwataka washiriki kufatilia kikamilifu mawasilisho yatakayotolewa ili kila mtu aone umuhimu wa kulinda mali, afya na uwekezaji kwa kutumia bidhaa za bima. Lakini pia aliwataka kuwa mabalozi wazuri wa bima kwa watu wanaowazunguka. 

Washiriki pia walipewa elimu ya bima na kupitishwa katika fursa mbalimbali zilizopo katika soko la bima ikiwemo kuwa wakala wa bima na washauri wa bima. Mawakala hao wa Forodha pia walinolewa kuhusu  sheria mbalimbali za bima pamoja na mifumo ya usajili na uhakiki wa bima (ORS na TIRAMIS) ya Mamlaka.  

Viongozi wa vyama hivyo pamoja na wanachama walipewa fursa ya kutoa maoni na kuuliza maswali mbalimbali yahusuyo  bima ambapo walizungumzia kuhusu bima ya kontena na utekelezaji wa malipo ya 3rd party cover. Maswali ambayo yalijibiwa kikamilifu na maafisa wa Bima na Sheria kutoka Mamlaka. Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Saqware pia aliwaalika viongozi wa vyama hivyo TAFFA na TACAS kufanya kazi kwa karibu na Mamlaka kwa kukutana na kutoa mapendekezo mbalimbali yatayosaidia soko la bima na forodha nchini na kuwahakikishia ushirikiano dhabiti. 

Meneja wa Kanda ya Mashariki Bw. Zakaria Muyengi aliwashukuru washiriki hao na kuahidi kuendelea kufanya semina na mikutano ili kuendelea kutoa elimu ya bima na fursa zilizopo katika soko. TIRA kanda ya Mashariki inahudumia mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro. 

#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA