ELIMU YA BIMA MKOANI MANYARA KATIKA MAONESHO YA BIASHARA YA TANZANITE
ELIMU YA BIMA MKOANI MANYARA KATIKA MAONESHO YA BIASHARA YA TANZANITE
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA )kupitia Kanda ya Kati Dodoma, inashiriki Maonesho ya Biashara ya Tanzanite mjini Babati mkoani Manyara. Lengo likiwa kutoa elimu ya bima, kusikiliza maoni mbalimbali na kujibu maswali yahusuyo bima.
Maonesho hayo yameanza rasmi tarehe 20 Octoba na yanatarajiwa kumalizika 30 .10. 2024 na leo Octoba 23, Mhe. Exaud S. Kigahe Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara amefungua rasmi Maonesho hayo na ametembelea banda la Mamlaka na kuelezwa majukumu mbalimbali yanayofanywa ikiwemo kusajili na kutoa leseni kwa watoa huduma za bima, kuandaa kanuni na miongozo mbalimbali katika soko, lakini pia kuhakikisha kila Mtanzania anaelewa kuhusu bima na kutumia bidhaa zake pamoja na kukuza soko la bima nchini.
Mhe. Waziri pia alielezwa na Maafisa Bima kutoka TIRA kwamba katika Maonesho hayo pia wanahamasisha wafanyabiashara kutumia huduma za bima ili kuhakikisha wanaendeleza biashara zao hata wanapokumbwa na majanga.
Aidha Mhe. Mgeni rasmi alisisitizaa juu ya kuhakikisha kuwa elimu inawafikia wananchi wote mjini na vijijini ili waweze kuhamasika kutumia huduma za bima.
#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA