Kikao kazi cha watumishi wa mamlaka ya usimamizi wa bima tanzania
Tarehe 29 Agosti 2023, watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) wamefanya kikao kazi cha wafanyakazi wote wakiongozwa na Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo A. Saqware ambaye ndiye Mwenyekiti wa Mkutano huo akishirikiana na Bi. Khadija I. Said, Naibu Kamishna wa Bima.
Katika kikao hicho mada mbalimbali ziliwasilishwa ambapo ni chachu ya Ufanisi mkubwa katika utendaji kazi wa Taasisi.
Mada zilizowasilishwa ni pamoja na Mpango wa Motisha (Incetives Schemes), Mada iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bi. Hawa Mniga, Sheria ya Bima, Kanuni na Miongozo mbalimbali, iliyowasilishwa na Mwanasheria Okoka Mgavilenzi, Utafiti wa Ripoti iliyowasilishwa na Ndugu. Samwel Mwiru, Mkurugenzi wa Masoko, Mipango na Utafiti, mada nyingine ilikuwa ni ya Tehama inayohusiana na taratibu za usajili na kaguzi mbalimbali kwa kutumia mfumo ambapo iliwasilishwa na ndugu Sefu Bakari akishirikiana na Bi. Tamali Mwakyosi, mada ya Usajili, Ukaguzi na Takwimu Bima iliyowasilishwa na Ndugu Bahati Ogola, mada inayohusiana na Mapato na Ujenzi iliyowasilishwa na Ndugu Andrew Msina, Mhasibu Mkuu kutoka Kurugenzi ya Uhasibu na mada ya mwisho ni kuhusu utunzaji wa kumbukumbu iliyowasilishwa na Bi. Bahati Likasa Mtunza Kumbukumbu Mwandamizi.
Majadiliano kwenye kikao hicho yameibua suluhu ya changamoto mbalimbali ambapo itasaidia katika ufanyaji kazi wenye tija kwenye sekta ya bima.
TIRA- kwa soko salama la Bima.