Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
HITIMISHO WIKI YA NENDA KWA USALAMA: ENDESHA SALAMA, UFIKE SALAMA, BIMA NI KINGA YAKO
30 Aug, 2024
HITIMISHO WIKI YA NENDA KWA USALAMA: ENDESHA SALAMA, UFIKE SALAMA, BIMA NI KINGA YAKO

WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI YAHITIMISHWA RASMI LEO

Ikiwa ni takriban wiki sasa tangu maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama yazinduliwe rasmi hatimaye tamati imefikia hii leo tarehe Agosti 30, 2024 ambapo wadau walioshiriki walikusanyika kwa pamoja katika hafla maalum ya kufunga rasmi maadhimisho hayo ambapo Naibu Waziri wa Uchukuzi na Kaimu Mwneyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Mhe. David Kihenzile alikua mgeni rasmi.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) ikiwa miongoni mwa wadau walioshiriki kikamilifu katika Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani 2024 ilipata fursa ya kupaza sauti kwa kutoa elimu ya bima na jinsi Sekta ya Bima inavyochangia katika kupunguza na kukabili madhara yanayotokana na ajali za barabarani kwa kutumia huduma ya Bima ya Vyombo vya Moto.

Kupitia kaulimbiu ya mwaka huu “Endesha Salama, Ufike Salama” Mamlaka imewafikia watanzania hususani wakazi wa Dodoma na mikoa mingine ya jirani kwa kiwakumbusha watanzania kuwa Usalama Barabarani ni la kwetu sote na kila mmoja akichukua hatua kiepuka ajali na kujikinga na madhara ya ajali inawezekana.

Mhe. Kihenzile amesema,“Elimu ambayo imekua ikitolewa tangu maadhimisho haya yafunguliwe rasmi ni chachu kwa madereva, waendesha pikipiki na watumiajji wote wa barabara. Kila mmoja anapaswa kwa namana moja au anyingine aguswe na suala la Usalama Barabarani. Ajali nyingi zinazotokea ni kwa sababu ya mapungufu ya kibanadamu. Serikali imeendelea kuchukua hatua ili kupunguza ajali zinazoweza kuzuilika kama vile ujezi wa barabara, matumizi ya mifumo ya kudhibiti mwendo wa magari na kudhibiti magari mabovu kuingia barabarani. Haya yote yanakwenda sawia na kila mmoja kuchukua tahadhari na hatua kuisalama”.

Mhe. Kihenzile ametoa rai kwa wadau na waahiriki wote wa Usalama Barabarani kuzingatia mkakati uliotolewa na Baraza la Usalama Barabarani. Wapanda pikipiki kuacha kuendesha pikipiki bila kupata mafunzo, bila kua na leseni barabarani, kuacha tabia ya kubeba abiria zaidi ya mmoja na kutoendesha bila kuvaa kofia ngumu. Watumiaji wengine wa barabara sote tuzingatie sheria za barabarani. Kwa wanaotumia magari kuacha tabia ya kushabikia mwendonkasi na kutokubali kusongamana kwenye magari.