Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
MAADHIMISHO YA BIMA YAFANA ZANZIBAR: “SERIKALI HAIWEZI KUFUMBIA MACHO MAGARI KUKOSA BIMA” – MHE. ZENA SAID
31 Aug, 2024
MAADHIMISHO YA BIMA YAFANA ZANZIBAR: “SERIKALI HAIWEZI KUFUMBIA MACHO MAGARI KUKOSA BIMA” – MHE. ZENA SAID

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima kupitia ofisi  ya Zanzibar leo jumamosi Agosti 31, imefanya maadhimisho ya Bima yaliyojumuisha matembezi ya hiari katika kukuza uelewa wa elimu ya bima visiwani humo.

Matembezi hayo yameanzia katika uwanja wa Mnara wa Kisonge, Michenzani mpaka uwanja wa Mao Zedong ambapo maadhimisho hayo yamefanyika. 

Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo ni Mhe. Mhandisi Zena Said, Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar. 

Mhe. Zena Said amesema “Serikali haiwezi kufumbia macho magari kukosa bima, tutafanya kazi na taasisi zingine wasiingie  ili wasiweze kuingia barabarani, pia nawaasa viongozi wa serikali kukatia bima mali zao” 

Tukio hilo pia lilihudhuriwa na Kamishna wa Bima Tanzania  Dr. Baghayo Saqware na Naibu Kamishna wa Bima Tanzania Bi. Khadija Said, pamoja na Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu na wadau mbalimbali katika sekta ya bima.

Matembezi ya Bima Zanzibar ni tukio la kila mwaka linaloandaliwa ili kuongeza uelewa kuhusu umuhimu Zanzibar. Tukio hili limekuwa likifanyika kwa ushirikiano wa wadau wa sekta ya Bima. 

#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA