Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Kuhusu Sisi

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima ya Tanzania (TIRA) ilianzishwa mwaka 2009 chini ya Kifungu cha 5 cha Sheria ya Bima, Cap. 394 .Chini ya usimamizi mkuu wa Wizara inayohusika na Fedha, TIRA ina jukumu la kuendeleza soko la bima na kuratibu sera pamoja na masuala mengine yanayohusiana na bima katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. TIRA pia inajukumu la kuhakikisha ufanisi na uadilifu katika sekta ya bima, na kuhimiza maendeleo ya sekta hiyo kwa faida ya wananchi na uchumi wa taifa.