Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Kamishna wa Bima asikiliza maoni ya wadau Maonesho ya Saba Saba, watoa huduma za bima wakiri kupata mafanikio makubwa
15 Jul, 2025
Kamishna wa Bima asikiliza maoni ya wadau Maonesho ya Saba Saba, watoa huduma za bima wakiri kupata mafanikio makubwa

TIRA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walishiriki Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara  Saba Saba yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 28 Juni hadi tarehe 13 Julai. Kampuni za bima na benki wakala wa bima zaidi ya arobaini walishiriki.

Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo Saqware alishiriki kwa kusikiliza mafanikio yaliyopatikana pamoja na maoni mbalimbali, ambapo watoa huduma za bima walikiri kupata mafanikio makubwa katika Maonesho hayo yakiwemo kupata wateja wapya lakini pia kutoa elimu kwa makundi ya vijana waliotaka kufahamu zaidi kuhusu bima. Pia ilikuwa fursa ya kujitangaza zaidi kwa jamii.

Dkt. Saqware pia aliwakumbusha kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia uwazi katika utedaji kazi. 

TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA