Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
KAMISHNA WA BIMA NDANI YA BANDA LA TIRA, APONGEZA JUHUDI ZA UTOAJI ELIMU YA BIMA
09 Aug, 2024
KAMISHNA WA BIMA NDANI YA BANDA LA TIRA, APONGEZA JUHUDI ZA UTOAJI ELIMU YA BIMA

Kamishna wa Bima, Dr Bhaghayo Saqware leo Agosti 8, 2024 ametembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) katika Maonesho ya Kilimo, (nane nane) ambapo rasmi yanamalizika leo. 

Dr. Saqware amepongeza timu ya waandaaji wa Maonesho haya kutoka TIRA na kupongeza juhudi zinazoendelea katika kutoa elimu ya bima, ili kila Mtanzania aweze kunufaika na huduma za Bima. 

Kamishna wa Bima,wakati wote amekuwa akisisitiza utoaji wa elimu ya Bima kumfikia kila mtanzania ili kuondokana na umaskini kwa kupata huduma sahihi za bima, 
zitakazomsaidia kuondokana na majanga na kuepuka umaskini.

#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA