Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
KAMPUNI ZA BIMA ZASISITIZWA  KUENDELEA KUTENDA HAKI KWA WAKATA BIMA.  
27 Oct, 2024
KAMPUNI ZA BIMA ZASISITIZWA  KUENDELEA KUTENDA HAKI KWA WAKATA BIMA.  

 Kampuni za bima nchini zimeaswa kuendelea kutenda haki kwa wakata bima ili kuendelea kujenga imani kwa wananchi kuhusu huduma hiyo muhimu kwa jamii.

Hayo yamesemwa leo tarehe 26 Oktoba 2024 na Naibu Kamishna wa Bima, Bi. Khadija I. Said alipotembelea Kijiji cha Bima kwenye Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Ruanda Nzovwe Jijini  Mbeya kuanzia tarehe 21-26 Oktoba 2024.

Miongoni mwa mambo aliyowaasa wadau hao wa Kampuni za bima ni pamoja na kuhakikisha wanawafidia wananchi  kwa wakati kulingana na miongozo pindi tu wanapopatwa na majanga bila kuwachelewesha.

Vilevile Naibu Kamishna wa Bima aliwapongeza wadau hao wa kampuni za bima kwa kuonesha uzalendo wa kuendelea kushiriki matukio mbalimbali ya Serikali likiwemo hili la utoaji wa elimu ya Fedha kwa Umma na kuwaasa kuendeleza ushirikiano huo ili kuimarisha soko la bima Tanzania.

TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA.