Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa - elimu ya bima kutolewa Tanga
18 Jan, 2026
Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa - elimu ya bima kutolewa Tanga

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) inashiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Fedha Kitaifa yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha kuanzia hapo kesho Januari 19 hadi 26 2026  katika Viwanja vya Usagara, mkoani Tanga, kwa lengo la kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu masuala ya fedha na umuhimu wa kutumia huduma rasmi za kifedha.

Kupitia maadhimisho hayo, TIRA inatarajia kutoa elimu ya bima kwa wananchi watakaotembelea banda lake, ikijumuisha maelezo ya kina kuhusu aina mbalimbali za bima zinazopatikana nchini, zikiwemo bima za vyombo vya moto, bima ya mali, bima ya maisha pamoja na Bima ya Afya kwa Wote. Elimu hiyo inalenga kuwawezesha wananchi kuelewa manufaa ya bima katika kulinda maisha, afya na mali dhidi ya hatari mbalimbali.

TIRA pia itashirikiana na wadau wadau wake ambao ni kampuni za bima za Serikali na binafsi katika kuongeza wigo zaidi wa wananchi kupata huduma za bima kwa karibu.Wananchi Wote wa Mkoa wa Tanga wanakaribishwa kupata elimu.

TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA