MAONESHO YA NANE NANE: PROF. RIZIKI SHEMDOE, KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI AIPONGEZA TIRA KWA KUENDELEA KUTOA ELIMU YA BIMA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki S. Shemdoe, ametembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzanka (TIRA) leo August 7, 2024 katika maonesho ya kilimo hapa Dodoma, ili kujionea kazi mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka bandani hapo
Prof. Shemdoe alielezwa majukumu mbalimbali ya TIRA na aina mbalimbali za bima na namna ambazo sekta ya bima inazitoa zikiwemo bima za mifugo ambazo zitawasaidia wafugaji kukinga mifugo dhidi ya majanga mbalimbali.
Prof. Shemdoe ameipongeza TIRA kwa kutoa elimu kwa umma na kuwataka kuendelea kutoa elimu hiyo kwa wafugaji na wavuvi ili waelewe na kuona umuhimu kukata bima.
TIRA pamoja na Kampuni za bima wanaendelea kutoa elimu ya bima mbalimbali zikiwemo bima za afya, bima za nyumba, bima za vyombo vya moto, bima za ukandarasi kwa wananchi wanaoendelea kutembelea maonesho haya.
Lengo likiwa kutoa uelewa na hatimaye wananchi wengi kunufaika na huduma ya bima.
#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA