MAONESHO YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA: “WAWEKEZAJI WA MADINI WAHAKIKISHIWE USALAMA WA MALI ZAO - Mkuu wa Wilaya Geita
MAONESHO YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA: “WAWEKEZAJI WA MADINI WAHAKIKISHIWE USALAMA WA MALI ZAO - Mkuu wa Wilaya Geita
Mkuu wa wilaya ya Geita Mhe. Hashim Abdallah Komba ameishauri Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kuhakikisha wawekezaji hasa kwenye sekta ya madini wanapatiwa bidhaa za bima zinazoweza kulinda mitaji yao pindi wanapopata majanga kwani wanawekeza fedha nyingi lakini wakati mwingine mgodi hukumbwa na changamoto hivyo wakiwa wanabima watafidiwa mali walizopoteza.
Mhe. Komba amezungumza hayo wakati alipotembelea banda la TIRA Octoba 8 2024 na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka, ameiasa Mamlaka kukazia sheria, kanuni na miongozo ya bima kama uhakiki wa usajili wa kampuni ili kulinda haki ya mkata bima.
Pia ametoa pongezi kwa Mamlaka kwa juhudi wanazozifanya kwa kushirikiana na wadau wake na kwa ubunifu wa Kijiji cha Bima kinachowaweka pamoja.
“ Kwani kuna ongezeko kubwa la kampuni za bima nchini, na hii inaonyesha sekta ya Bima inakuwa na ni jambo la kujivunia.” Amesema Mhe. Komba.
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) inashiriki katika Maonesho ya 7 ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita kuanzia Octoba 2 - 13 katika viwanja vya Bombambili ambapo maonesho hayo yanatarajiwa kufungwa rasmi Octoba 13 na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA.