Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
MBEYA: OFISI YA KANDA, NYANDA ZA JUU KUSINI KATIKA MAONESHO YA NANE NANE
08 Aug, 2024
MBEYA: OFISI YA KANDA, NYANDA ZA JUU KUSINI KATIKA MAONESHO YA NANE NANE

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), kupitia ofisi zake za Kanda ya Nyanda za Juu Kusini inashiriki Maonesho ya Nane nane, katika viwanja vya Mwakangale jijini humo. Rasmi yatamalizika leo Agosti 8, 2024 na kitaifa yanafanyikia mkoani Dodoma ambapo yafungwa rasmi na Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

TIRA imeendelea kutoa elimu ya Bima kwa wakazi wa Nyanda za Juu Kusini ambapo ofisi zetu za kanda zilizopo mkoani Mbeya zinahudumia pia mikoa ya jirani kama Songwe na Njombe.

Bi. Neema Lituli ambaye ni Meneja wa Mamlaka kanda hiyo amewaasa watanzania kuendelea kufika katika ofisi zao kwa masuala mbalimbali yahusuyo bima na kusisitiza wataendelea kuhakikisha kila mwananchi wa Nyanda za Juu kusini anafahamu kuhusu umuhimu wa bima na kunufaika na huduma hiyo.

#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA