Uzinduzi wa Miongozo ya Bima tarehe 03 Agosti 2023
Tarehe 03.08.2023 Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imefanya uzinduzi wa Miongozo Mipya mitatu ya bima ambayo ni:
- Miongozo ya Usimamizi wa Ubakizaji wa Bima na Bima Mtawanyo.
- Miongozo ya Bima ya Afya na Usajili wa Watoa Huduma za Afya.
- Miongozo ya Utoaji Ithibati kwa Warekebishaji na Watengenezaji wa Vyombo vya Moto wanao wahudumia sekta ya Bima.
Uzinduzi wa Miongozo hiyo umefanyika katika ukumbi wa Mtakatifu Gasper jijini Dodoma. Ambapo Mgeni rasmi alikuwa Bi. Jenifa C. Omolo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha-Huduma za Hazina. Aidha, Bw. Abubakar Ndwata, Mkurugenzi wa Usimamizi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania alishiriki uzinduzi huo kwa niaba ya Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo A. Saqware. Uzinduzi huo pia umehudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya bima Nchini na baadhi ya Watumishi wa Mamlaka (TIRA).
Miongozo hiyo inalenga kuimarisha usimamizi na kuendeleza sekta ya bima Nchini.
Ili kupata nakala kamili ya miongozo hii unaweza kutembelea tovuti rasmi ya TIRA ambayo ni: (www.tira.go.tz) au kwa kubofya link hapo chini:
“TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA”