Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
PWANI: TIRA YATOA ELIMU YA BIMA IKWIRIRI, YADHAMINI NA KUSHIRIKI MASHINDANO YA POLISI JAMII CUP
06 Sep, 2024
PWANI: TIRA YATOA ELIMU YA BIMA IKWIRIRI, YADHAMINI NA KUSHIRIKI MASHINDANO YA POLISI JAMII CUP

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), kupitia Kanda ya Mashariki leo Ijumaa Agosti 6, 2024 imetoa elimu ya bima kwa wananchi wa kata ya Ikwiriri wilayani Rufiji, mkoa wa Pwani. 

Utoaji wa elimu kuhusu Taasisi, majukumu yake na faida za kutumia huduma za bima ulitolewa na Afisa Bima Ndg. Joseph Mfoi pamoja na Afisa Uendelezaji Soko Mwandamizi Ndg. Collins Nyimbo, kwa wananchi walioshiriki mashindano hayo ya Mpira wa Miguu kwa jina la Polisi Jamii Cup, uwanja wa Mabatini Ikwiriri. 

TIRA pia ni mdhamini wa mashindano hayo ambapo Mratibu Mkuu wa Polisi Jamii Cup,  ACP J. B Ibrahim ameishukuru Mamlaka kwa udhamini na ushirikiano wa mara kwa mara. 

Lengo la ushiriki huo na uhamasishaji wa huduma za bima ni kuendelea kuhakikisha kila Mtanzania anafahamu kuhusu bima na kutumia huduma za bima ili kuweza kurudi katika hali ya mwanzo pale anapopata majanga. 

TIRA kanda ya Mashariki inahudumu mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro. Mashindano hayo yanatarajiwa kumalizika kesho Agosti 7, 2024 ambapo Mamlaka pia itatoa elimu bima na namna ya kutumia mifumo ya TIRA. 

#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA ‎