Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Raisi mwinyi aielekeza TIRA kutekeleza mabadiliko ya sheria ya fedha .
14 Aug, 2022
Raisi mwinyi aielekeza TIRA kutekeleza mabadiliko ya sheria ya fedha .

Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Husein Mwinyi ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA) kutekeleza mabadiliko ya Sheria ya Fedha Na. 05 ya mwaka 2022 kwa manufaa ya wananchi na kuwakinga dhidi ya majanga.

Hayo ameyasema, Ikulu mjini Unguja, mara baada ya kukutana na Ujumbe wa wataalamu wa sekta ya bima ukiongozwa na Kamishna wa Bima nchini Dkt. Baghayo Saqware.

"Niwataka mshirikiane na TAMISEMI, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Wakala wa Meli Zanzibar (ZMA), Ushirika la Bandari Zanzibar (ZPC) na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kuhakikisha mabadiliko haya hususan katika mizigo inayoagizwa kutoka nje ya nchi, yanakuwa na faida kwa uchumi wa nchi yetu na wananchi kwa ujumla" alisema Dkt. Mwinyi.

Pamoja na maelekezo hayo, Dkt. Saqware alimkabidhi Mhe. Rais Mwinyi miongozo mitatu ya sekta ya bima yenye lengo la kuongeza wigo wa upatikanaji huduma za bima iliyozinduliwa hivi karibuni.

Akimkabidhi miongozo hiyo, Dkt. Saqware alitoa shukrani za dhati kwa Mhe. Rais kukubali na kuwa Mgeni Rasmi katika mkutano wa Mwaka wa kampuni za bima Afrika (Africa Insurance Industry Retreat ulioandaliwa na Chuo cha Bima na Hifadhi wa Jamii Africa - ACISP) uliyofanyika Januari 25-28, 2022. Pamoja na hilo amewasilisha ombi kwa Mhe. Rais la kuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano wa Mwaka wa Umoja wa Wanabima wa Mashariki na Kusini mwa Afrika (OESAI) utakofanyika tarehe 28-31 Agosti 2022.

“Hii miongozo imekuja wakati muafaka, kwani ni matarajio ya serikali kuwa wananchi wote bila kujali vipato ama imani zao wanajumuishwa katika mfumo wa fedha na naamini utekelezaji wa muongozo wa Takaful na miongozo mingine itatoa fursa za ajira kwa vijiana wengi nchini” alisema Dkt. Mwinyi.