Raisi Mwinyi ataka kampuni za bima kukinga miradi mikubwa
Raisi Dkt. Mwinyi ameziagiza kampuni za Bima Africa kuhakikisha zinatoa kinga ya bima miradi mikubwa na wananchi wenye kipato cha chini. Dkt. Mwinyi amesema hayo wakati akifungua Mkutano wa 44 wa Umoja wa Wataalamu wa Bima Mashariki na Kusini mwa Afrika (OESAI) uliyofanyika mjini Zanzibar.
"Soko letu la bima lina fursa nyingi kwa sasa na serikali imeamua kubadilisha sheria katika baadhi ya maeneo muhimu ili kutoa kinga na kutoa fursa kwa biashara kufanyika kwa ufanisi nchini" alisema Dkt. Mwinyi.
Maeneo yanayopaswa kupewa kipaumbele ni shughuli za uchumi na kijamii zitokanazo na uchumi wa blue, uchimbaji wa madini na mafuta, miradi mikubwa ya ujenzi na shughuli za kilimo.
Akieleza maendeleo ya soko la bima nchini Dkt. Baghayo Saqware amesema kuwa Mamlaka ya Bima inaendelea kuhakikisha inatoa miongozo na kanuni zikazoendelea na kuvutia wawekezaji nchini.
"Tumezindua miongozo mitatu hivi karibu, serikali imefanya mabadiliko yaliyogusa uuzaji wa bima za lazima. Soko letu pia, linaemdelea kuhakikisha linakuwa na taswira chanya" alisema Dkt. Saqware.