Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
RC KUNENGE: BIMA NI JAMBO LA MSINGI NI MUHIMU KUTOA UELEWA, ZIARA YA TIRA MKOA WA PWANI
26 Aug, 2024
RC KUNENGE: BIMA NI JAMBO LA MSINGI NI MUHIMU KUTOA UELEWA, ZIARA YA TIRA MKOA WA PWANI

​​​​​
Agosti 22, 2024 Ziara ya TIRA mkoa kwa mkoa imefika kwa Mhe. Abubakar Kunenge Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambapo wamekubaliana kuweka mikakati ya pamoja ya kuelimisha Wananchi kuhusu bima.

Akizingumza wakati wa utoaji wa taarifa kuhusu bima Kamshna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware amesema TIRA inawajibu wa kuelimisha kuhusu bima huvyo kupitia kwa Mkuu wa Mkoa inaweza kupata fursa ya kuwafikia wananchi wengi wakiwemo watumishi wa serikali, viongozi wa serikali za mitaa na mabaraza ya madiwani.

Kwa upande wake RC kunenge ameahidi kutoa ushirikiano na kusema bima ni jambo la msingi hivyo ni muhimu watu kuwa na uelewa. Kunenge alielezea namna ukanda huo wa Pwani unavyokua kwa kasi kwa kuwa na ongezeko kubwa la viwanda vikubwa na vya kati hivyo kuwepo na uhitaji mkubwa wa bima ili kukinga uwekezaji huo dhidi ya majanga.

Kwenye ziara hiyo Kamishna pia aliambatana na Naibu Kamishna Bi. Khadija Said pamoja na viongozi wengine wa TIRA waandamizi.