Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
SEKTA YA BIMA IMETENGENEZA FURSA YA AJIRA NA VIPATO KWA WANANCHI – Bw. Frank Shangali Meneja TIRA
24 Oct, 2024
SEKTA YA BIMA IMETENGENEZA FURSA YA AJIRA NA VIPATO KWA WANANCHI – Bw. Frank Shangali Meneja TIRA

Katika kuhakikisha elimu ya bima inatolewa kwa jamii, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) inafanya jitihada mbalimbali kumfikia kila mwananchi mjini na vijijini. Kwa kuzingatia hilo Mamlaka kupitia Kanda ya Kati Dodoma inashiriki Maonesho ya Wafanyabiashara ya Tanzanite katika viwanja vya Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara. Maonesho hayo yalianza rasmi Octoba 20 na yanatarajiwa kumalizika Octoba 30 2024.

Bw. Frank Shangali ni Meneja wa TIRA kanda ya kati, kanda hiyo inahudumu mikoa ya Dodoma, Manyara na Iringa. Leo Octoba 24, 2024 Bw. Shangali alifanya kipindi na redio FM Manyara na kutoa ufafanuzi kwa maswali yaliyoulizwa katika kipindi hicho lengo likiwa kuhakikisha elimu ya bima inapenya kwa wananchi hata ambao hawajaweza kuhudhuria Maonesho hayo. Ambapo aliweza kueleza mambo mbalimbali kama ifuatavyo;

Ni yapi majukumu ya TIRA?

TIRA ina  majukumu mbalimbali  ambayo ni kusajili na kutoa leseni kwa watoa huduma za bima, kuandaa na kutoa kanuni na miongozo mbalimbali ya kusimamia soko la bima, kutoa elimu ya bima kwa umma,kulinda haki za mteja wa bima, kuendeleza,kusimamia uhimilivu  na uendelevu wa soko la bima na kushauri serikali

TIRA ina mikakati gani ya muda mrefu kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya bima?

Bw. Shangali alieleza ushiriki wa Mamlaka kwenye Maonesho, majukwaa, semina na mikutano mbalimbali na wananchi, taasisi za serikali na binafsi ambapo maafisa mbalimbali wa Mamlaka hutoa elimu ya bima. Pia aligusia ziara za Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware za mkoa kwa mkoa katika kuhakikisha viongozi wa mikoa wanapata elimu hiyo na kuhamasisha wananchi kutumia bidhaa hizo. Pia matumizi ya vyombo vya habari kama redio, televisheni na magazeti katika kutoa habari kwa wananchi.

Meneja pia alielezea umuhimu wa bima ya vyombo vya moto ambapo mathalani chombo cha usafiri wa umma kimepata majanga ni wakati bima inapoingia na kusaidia, kwasababu gharama ni kubwa bila kuwa na bima ya chocho cha moto.

Lakini pia alizungumzia Sheria ya Bima ya Afya kwa wote ambayo italeta unafuu kwa kila mwananchi, kwasababu kila mmoja ataweza kutumia huduma ya bima ya afya kutokana na kiasi cha pesa aliyonayo.

Mwisho kabisa aliwakaribisha wananchi wa Babati na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi katika banda la Mamlaka ili kuweza kupata elimu sahihi ya bima lakini pia kuelezwa fursa zilizopo katika sekta ya bima ikiwemo kuwa wakala wa bima na mshauri wa bima kwa masharti nafuu hivyo kujiongezea kipato kwa  mapato yatokanayo na fursa hiyo.

#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA