Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
SIKU YA BIMA YAFANA: WADAU SEKTA YA BIMA WAKUTANA MKUTANO MKUU DODOMA
14 Sep, 2024
SIKU YA BIMA YAFANA: WADAU SEKTA YA BIMA WAKUTANA MKUTANO MKUU DODOMA

Mkutano wa kila mwaka wa siku ya bima umefanyika leo Septemba 14, 2024 jijini Dodoma. Wadau mbalimbali katika sekta ya bima wamekutana ambapo Mgeni Rasmi ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum Mhe. Dorothy Gwajima (MP).

Mkutano huu  ni mwendelezo wa Wiki ya Bima 2024 na umeandaliwa na Taasisi ya Bima (IIT) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA)  ukiwa na lengo  la kukutanisha wadau wa bima wakiwemo kampuni za bima, vyuo/taasisi za bima na watumiaji wa huduma za bima, kujadili mambo mbalimbali kuhusu sekta ya bima nchini. 

Katika hotuba yake Mhe. Gwajima ameipongeza TIRA kwa majukumu yake katika kutoa elimu ya bima Tanzania na kusisitiza elimu ya bima kutolewa zaidi kwa jamii.  “Kaeni na vyuo vya Maendeleo ya Jamii wapewe elimu (wanachuo) ili kuongeza sauti ya sekta ya bima’’

Mhe. Gwajima pia alisisitiza “Kauli mbiu hii ya mwaka huu “Bima jumuishi: bidhaa zinazokidhi mahitaji na usambazaji wa Kiteknolojia” ikatufanye  tuwe na tafakuri ya mpango mkuu wa maendeleo ya sekta ya fedha 2020 – 2030 kwa sekta ndogo ya bima, sambamba na maelekezo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.