“Taasisi za Umma na Mashirika, Zishiriki Michezo ya SHIMMUTA kikamilifu” Dkt. Doto Biteko - Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati
Mashindano ya Michezo ya SHIMMUTA yamefunguliwa rasmi leo Novemba 18, 2024 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko katika viwanja vya Usagara mkoani Tanga.
Akifanya ukaribisho wa mashindano hayo Mwenyekiti wa SHIMMUTA Bi. Roselyne Mathew Massam amesema lengo la mashindano hayo ni kuleta hamasa na ari kwa wafanyakazi lakini pia kuimarisha afya ya mwili na akili. Pia ameongeza takwimu zinaonyesha mwaka huu timu zimeongezeka kutoka 57 mwaka jana hadi timu 96 na washiriki kutoka 3608 mwaka jana hadi 4720 mwaka huu.
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imeshiriki mashindano hayo kwa michezo ya jadi ikiwemo karata, riadha, bao, draft, darts na kukimbia Afisa Utumishi Mwandamizi Joel Ahaz kwa niaba ya Mkurugenzi Utawala na Rasilimali Watu Bi. Hawa Mniga amesema “ Tunayo furaha kushiriki kwa mara ya kwanza mashindano haya ambapo kwa upande wa darts na bao timu zilifanikiwa kufika hatua ya robo fainali lakini pia tuna michezo mingine iliyobaki ya kukimbia na gunia na riadha na tunatarajia ushundi”.
Kwa upande wa Mgeni Rasmi, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amezitaka taasisi za umma na mashirika kuhudhuria michezo hii kwa wingi bila visingizio na kuzitaka zitenge bajeti mapema lakini pia alihimiza Wizara husika kutoa Sera ya Michezo mahali pa kazi.
Viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Mhe. Jumaa Aweso Waziri wa Maji na Mbunge wa Pangani, Mhe. Gerson Msigwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo , Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Batilda Buriani na Mbunge wa Tanga Mjini Mhe. Ummy Mwalimu.
#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA