Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania iliwapokea Mabalozi wa Bima.
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), tarehe 06 Machi 2023 iliwapokea Mabalozi wa Bima ambao ni Mheshimiwa Mhandisi Zena Said (kulia) ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la mapinduzi Zanzibar na Mhe. Wanu Hafidh Ameir (kushoto) ambaye ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano. Mabalozi hao wamekutana na Kamishna wa Bima Dkt.Baghayo Saqware(katikati) na Naibu Kamishna Khadija Said. Aidha Ndg. Rajab Kakusa CEO wa TANRE alihudhuria mkutano huo. Mabalozi wa Bima hao ambao ni watatu ikiwa ni pamoja na Mhe.Japhet Hasunga (hayupo pichani) wameanza majukumu yao ya kuungana na TIRA na wadau wa Sekta ya bima katika eneo la kutoa uelewa na kuishauri Mamlaka ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kikao cha Makatibu Wakuu cha Septemba 2022 kilichofanyika jijini Dodoma. Kwa upande wake Dkt.Saqware amewapongeza Mabolozi wa Bima kwa kuona umuhimu wa kuungana na TIRA ili kuongeza kasi ya maendeleo ya Sekta ndogo ya Bima.
TIRA kwa Soko Salama la Bima.